ULAYA

Arsenal wawapa raha mashabiki

Lukas Podolski
Lukas Podolski

Mtanange wa ligi kuu Ulaya imeendelea hapo jana kati ya timu mbalimbali ambapo timu ya Arsenal imefanikiwa kutikisa nyavu mara tatu dhidi ya Fulham ambao wao wameingia nyavuni mara moja na hivyo Arsenal kuibuka na ubingwa wa magoli 3-1 huku Liverpool wakipata ushindi kwa mara ya pili na Aston Villa. 

Matangazo ya kibiashara

Magoli ya Arsenal yalipatikana baada ya mchezaji Lukas Podolski kutikisa nyavu mara mbili huku kiungo wa kati Olivier Giroud akishindilia msumari wa tatu maumivu kwa Fulham jambo lililowapa raha mashabiki wa Arsenal.

Liverpool wameenda pointi sawa na Chelsea wakishika nafasi ya juu katika msimamo baada ya kushinda goli moja kwa nunge goli la pekee lililofungwa na Daniel Sturridge.