Arsenal yasonga mbele michuano ya UEFA kwa kuilaza Fernerbahce mabao 2 kwa 0

Arsenal FC ya Uingereza imefuzu katika ligi ya soka barani Ulaya baada yakuifunga Fernerbahce ya Uturuki mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa mzungumzo wa pili uliochezwa Jumanne usiku.

Matangazo ya kibiashara

Mabao yote mawili ya Aaron Ramsey yaliihakikishia Arsenal nafasi katika ligi hiyo ya UEFA ambayo imekuwa ikishiriki kwa miaka 16 iliyopita.

Arsenal inafuzu kwa jumla ya mabao 5 kwa 0 baada ya kupata ushindi wake wa kwanza wa mabao 3 kwa 0 jijini London Uingereza na kufuzu katika michuano hiyo.

Fenerbahce imeshindwa kufuzu kipindi hiki ikijiandaa kupokea ripoti kutoka kwa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuhusu rufaa iliyowasilisha baada ya kupigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi zozote barani Ulaya kwa kosa la kupanga mechi.

Mbali na Arsenal, mabingwa mara saba wa taji hili la Ulaya AC Milan ya Italia wanashuka dimbani siku ya Jumatano kumenyana na PSV Eindhoven ya Uholanzi katika uwanja wao wa nyumbani wa San Siro.

Ac Milan ilijiunga na Arsenal na vlabu vingine 20 kumenyana katika hatua ya makundi kusaka nafasi ya kufuzu katika hatua ya pili ya michuanio hiyo msimu huu.

Vllabu hivyo viwili vilitoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa kwanza wiki mbili zilizopita na mchuano wa Jumatano ni muhimu sana kwa timu zote kwa sababu zinahitaji ushindi.

Mbali na mchuano huo, mechi zingine zinazochezwa ni kati ya
Real Sociedad na Lyon huku Zenit St Petersburg ikimenyana na Pacos Fereira.