KIKAPU

Robo fainali ya michuano ya mchezo wa kikapu barani Afrika yaanza

Michuano ya robo fainali ya kusaka ubingwa wa Afrika katika mchezo wa kikapu kwa upande wa wanaume inaanza kutimua vumbi siku ya Jumatano jijini Abidjan nchini Cote Dvoire.

Matangazo ya kibiashara

Angola na Morroco wanamenyana katika robo fainali ya kwanza, huku Misri wakicheza na Capeverde katika mechi ya pili.

Wenyeji Cote Dvoire wanachuana na Cameroon, huku Nigeria wakipepetena na Senegal katika robo fainali ya mwisho.

Wawakilishi wa Afrika Mashariki na Kati katika mashindano hayo Rwanda waliondolewa katika hatua ya kufuzu baada ya kufungwa na Sengel kwa vikapu 67 kwa 57, huku Nigeria wakiwashinda Jamhuri ya Afrika ya kati kwa vikapu 112 kwa 75.

Angola wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huu nao waliwashinda Mali kwa vikapu 82 kwa 36 siku ya Jumatatu huku Misri ikiifunga Tunisia vikapu 77 kwa 67.

Rwanda na Tunisia zinachuana katika mchuano wa kuwania nafasi ya tisa katika mashindano haya ya bara Afrika siku ya Jumatano.

Nusu fainali ya michuano hii itachezwa siku ya Ijumaa huku fainali ikipigwa siku ya Jumamosi.

Mataifa 16 yalifuzu katika mashindano haya ya barani Afrika katika makala ya 27 ya michuano hii na washindi watatu wa kwanza watafuzu katika kombe la dunia mwaka ujao.