SOKA

Droo ya ligi ya Europa barani Ulaya yatagazwa

Droo ya ligi ya soka ya Europa barani Ulaya imetolewa siku ya Ijumaa na vlabu kugawanywa katika  makundi 12.

Matangazo ya kibiashara

Klabu ya Swansea ya Uingereza itamenyana na Valencia ya Uhispania katika kundi la A huku Tottenham Hotspur pia ya Uingereza ikipangwa katika kundi moja na Anzhi Makhachkala ya Urusi.

Wachambuzi wa soka wanasema kuwa Swansea itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Valencia, huku Tottenham Hotspurs wakionekana kupata timu nyepesi na hivyo wanatarajiwa kufuzu kwa urahisi.

Hivi ndivyo vlabu mbalimbali vilivyopangwa katika ligi kuu ya Europa

Kundi A: Valencia, Swansea, Kuban, St Gallen

Kundi B: PSV Eindhoven, Dinamo Zagreb, Chornomorets Odesa, Ludogorets

Kundi C: Standard Liège, Salzburg, Elfsborg, Esbjerg

Kundi D: Rubin, Wigan Athletic, Maribor, Zulte Waregem

Kundi E: Fiorentina, Dnipro, Paços Ferreira, Pandurii

Kundi F: Bordeaux, APOEL, Eintracht Frankfurt, Maccabi Tel Aviv

Kundi G: Dynamo Kyiv, Genk, Rapid Wien, Thun

Kundi H: Sevilla, Freiburg, Estoril, Liberec

Kundi I: Lyon, Betis, Guimarães, Rijeka

Kundi J: Lazio, Trabzonspor, Legia, Apollon

Kundi K: Tottenham, Anzhi Makhachkala, Sheriff, Tromsø

Kundi L: AZ Alkmaar, PAOK, Maccabi Haifa, Shakhter Karagandy

Mbali na droo hiyo mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Ulaya Bayern München ya Ujerumani watamenyana na mabingwa watetezi wa ligi ya Europa Chelsea kutoka Uingereza kuwania taji ya UEFA Super Cup.

Mchuano huo utachezwa Ijumaa usiku utawakumbusha mashabiki wa soka barani Ulaya na nchini Uhispani upinzan kati ya Kocha mpya wa Chelsea Jose Mourihno na Pepe Guardiola wa Bayern Munich.

Kabla ya kuhamia katika vlabu hivyo Mourihno alikuwa mkufunzi wa Real Madrid huku Guardiola akiwa na Barcelona zote za Uhispania.

Mourihno amesema kuwa haangalii rekodi nzuri aliyonayo Guardiola dhidi yake walipokuwa nchini Uhispania na ana uhakika vijana wake watafanya vizuri katika mchuano huo.

Guardiola kwa upande wake anasema kuwa anamheshimu sana Mourihno kwa kile alichokisema ana upeo mkubwa wa kukipanga kikosi chake vizuri ambacho si rahisi kufungika.

Mwaka 2004 Mourinho alipokuwa na klabu ya Chelsea, aliishinda Bayern katika hatua ya mzunguko wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya na kuishinda katika fainali ya UEFA mwaka 2009 alipokuwa na InterMilan ya Italia.

Hata hivyo, mwaka 2011 Mourinho akiongoza klabu ya Real Madrid alifungwa na Bayern Munich katika mchuano wa nusu fainali ya mchuano ya UEFA.