SOKA-ULAYA

Bayern Munich watwaa ubingwa wa taji la UEFA Super Cup

www.supersport.com

Mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Ulaya Bayern Munich ya Ujerumani wameibuka na ushindi wa taji la UEFA Super Cup baada ya kupata ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya wapinzani wao mabingwa watetezi wa ligi ya Europa Chelsea kutoka nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Bayern iling'ara katika mchuano huo wa fainali uliopigwa usiku wa ijumaa kupitia mikwaju ya penati baada ya mtanange huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika dakika za nyongeza.

Kiungo wa kati wa Chelsea Ramires alitolewa nje katika dakika ya 85 baada ya kupigwa kadi ya njano mara mbili hivyo kupelekea kikosi cha Mourinho kubakia na wachezaji 10 pekee.

Dakika tisini za awali zilitamatika kwa sare ya bao 1-1.

Mkwaju ya penati ililazimika kupigwa baada ya Javi Martinez wa Bayern kupachika bao katika dakika za lala salama hivyo kufanya sare ya mabao 2-2 katika dakika ya 121.

Ushindi huo umekuwa ni faraja kubwa kwa Guardiola aliyechukua jukumu la kuinoa Bayern mwezi June mwaka huu akitokea Barcelona ambapo aliiwezesha kuibuka na jumla ya mataji 14 katika miaka yake minne ya kukinoa kikosi hicho.