SOKA-ENGLAND

Kocha wa Manchester City aahidi makubwa katika ligi kuu Uingereza msimu huu

Baada ya Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull city katika mtanange wa kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Kocha wa Man City Manuel Pellegrini amewaahidi mashabiki wake kuhakikisha kikosi chake kinaendelea kufanya vizuri zaidi na kunyakua ubingwa katika msimu huu.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Bao la kwanza la City lilipachikwa kimiani kwa pasi ya kichwa na Alvaro Nagredo katika dakika ya 65 wakati la pili lilipachikwa na Yaya Toure katika dakika ya 90 kabla ya kutamatishwa kwa mchezo huo.

Ushindi huo wa siku ya jumamosi katika dimba la Etihad umekuwa ni faraja kwa City ambao juma lililopita walitandikwa mabao 3-2 na Cardiff ambayo imepanda daraja msimu huu.

Katika mechi yao ya kwanza City walifanya vyema baada ya kupata mabao 4-0 dhidi ya Newscastle katika mechi yao ya kwanza.

Ligi kuu ya Uingereza inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi hii jumapili hii ambapo Arsenal watachuana na Tottenham, Liverpool na Manchester United wakati Swansea wataumana na West Bromwich Albion.