GHANA

Klabu nchi Ghana zatakiwa kuwalipia wachezaji hifadhi ya jamii, bima

RFI

Klabu za soka nchini Ghana zimetakiwa kuwalipia wachezaji michango fedha katika mashirika ya hifadhi ya jamii na wafanyakzi wengine wanaoajiriwa katika klabu hizo. 

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa katika kongamano la mwaka la chama cha klabu za ligi ya soka nchini Ghana.

Shirika la hifadhi ya jamii la Ghana limesema kuwa klabu hizo zinalazimika kutekeleza wajibu huo ambao upo kisheria na endapo klabu itashindwa kufanya hivo hatua zitachukuliwa.

Shirika hilo limesema kuwa hatua hizo zinachukuliwa ili kuwasaidia wachezaji kuwa na bima kwa sababu chochote kinaweza kutokea katika michezo.

Klabu zitakiwa kutoa michango mfululizo na kukamilisha taratibu za bima kila mwaka.