COTE D'IVOIRE

Yaya Toure akanusha kugombana na Drogba, atoboa siri

REUTERS/Murad Sezer

Mchezaji kiungo wa klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Toure ametoboa siri na kusema kuwa kama angesikiliza ushauri wa timu ya Taifa ya Cote D'ivoire Didier Drogba basi angewahi kuwa mchezaji wa Chelsea.

Matangazo ya kibiashara

Yaya Toure amesema kuwa wakti Drogba akiichezea Chelsea mwaka 2005 alikua akimshawishi mara kwa mara ajiunge na klabu hiyo na kama angekubali basi angejiunga na timu.

Katika mahojiano na kituo cha televishen cha RTI Toure na Drogba walizungumzia tuhuma kwamba wachezaji hao hawana maelewano na ndiyo maana timu yao ya taifa imekua ikifanya vibaya.

Yaya Toure amesema kuwa yeye hana sintofahamu na mchezaji Drogba na amekuwa akishirikiana vizuri na kapteni huyo wa timu.
Toure amekanusha vikali habari kwamba ana ugonvi na mchezaji na kusema kuwa.

Drogba amekuwa rafiki wake wa karibu kwa kipindi kirefu tofauti na watu wanavyosema.

Mchezaji huyo alihoji kuwa itawezekanaje adui yake amshauri kuhamia timu anayozea ilihali kuna tofauti baina yao na kuongeza kuwa kamwe hawajawahi kugombana na hawatakuja kugombana hata siku moja.

Toure amesema kuwa Drogba ni rafiki yake, ndugu yake na mshauri wake hivyo hawawezi kuwa maadui.