Marekani

Andy Murray afanikiwa kutinga hatua ya robo mashindano ya US Open

REUTERS/Suzanne Plunkett

Bingwa mtetezi wa mashindano ya tenisi ya US Open Andy Murray amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano baada ya kumlaza Denis Istomin wa Uzbekistan.

Matangazo ya kibiashara

Kwa ushindi huo Andy Murray sasa atakabiliana na Stanislas Wawrinka katika hatua hiyo ya robo fainali siku ya Alhamisi ya wiki hii.

Andy Murray mwenye umri wa miaka 26 alipata wakati mgumu na hatimaye kufanikiwa na ushindi wa seti za 6-7 (5-7) 6-1 6-4 6-4.

Andy Murray alimsifu mpinzani wake Denis Istomin na kusema kuwa alimpa wakati mgumu kutokana na umahiri wake kimchezo.

Mchezaji huyo amesema kuwa kwa sasa anaelekeza nguvu katika mchezo wake wa robo fainali ili apate ushindi katika harakati zake za kutetea ubingwa.