HISPANIA

Gareth Bale hajahakikishiwa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza Real Madrid

REUTERS/Paul Hanna

Mchezaji mpya wa Real Madrid Gareth Bale hajahakikishiwa moja kwa moja kuwa atakuwa muda akianza katika kikosi cha kwanza pamoja na yeye kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa kuliko wote baada ya kununuliwa hivi karibuni na klabu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kocha msaidizi wa Real Madrid Paul Clement amesema kuwa Gareth Bale licha ya kununuliwa kwa gharama kubwa ya zaidi ya paundi mili0ni 85 haimanishi kuwa kila mara atakua akianza katika kikosi cha kwanza.

Paul Clement amesema kuwa ndani ya klabu hiyo kuna ushindani mkubwa hivyo Gareth Bale pamoja nawachezaji wengine hawawezi wakahakikishiwa namba kulingana na hali halisi.

Kocha huyo msaidizi amesema kuwa mambo yatakuwa yakibadilika kulingana na mahitaji ya wakati huo na kwa namna kocha mkuu ataona inafaa.

Paul Clement ameongeza kusema kuwa kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti anafahamu namna ambavyo atamtumia mchezaji Gareth Bale lakini si lazima awe na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.