GHANA-SENEGAL

Timu za taifa za Ghana na Senegal zahitaji pointi moja kusonga mbele kuelea fainali za Kombe la Dunia

RFI

Timu za taifa ya soka za Ghana na Senegal ni miongoni mwa timu tano ambazo zinahitaji alama moja mwishoni mwa juma hili kufuzu katika mzungunko wa mwisho wa kusaka tiketi yta kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa saba yanatarajiwa kufuzu mwishoni mwa juma hili na kujiunga na Algeria, Misri na Cote Dvoire ambazo tayari zimeshafuzu kwenye timu kumi kabla ya kuchujwa na kupatikana timu tano wakilishi.

Cameroon, Ghana, Nigeria, Senegal na Tunisia zote zitakuwa nyumbani na zinahitaji sare ili kusonga mbele.

Kesho Ijumaa mchuano unasubiriwa ni kati ya Ghana na Zambia mchuano ambao wenyeji Ghana watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Baba Yaro mjini Kumasi.

Kikosi cha Ghana kikiongozwa na wachezaji kama Dede Ayew, Kevin-Prince Boateng na Michael Essien wanatarajiwa kuongioza kikosi cha Black Stars.

Kikosi cha Chipolopolo chini ya Kocha Harve Renard kinahitaji ushindi dhidi ya wenyeji wao ili kufuzu katika hatua ya mwisho lakini kikosi hicho kitakosa hudumu ya mshmabulizi Jacob Mulenga ambaye ana jeraha.