UINGEREZA-MOLDOVA

Uingereza kumenyana na Moldova mbio za fainali za Kombe la Dunia

Timu ya taifa ya soka ya Uingereza Ijumaa wiki hii itakuwa nyumbani kumenyana na Moldova katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la dunia.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Uingereza watakuwa uwanjani wakisaka ushindi wa kuwapa uongozi katika kundi lao ambao wapo katika nafasi ya pili kwa alama 12 nyuma ya Montenegro ambayo ina alama 14.

Baada ya mchuano wa kesho siku ya Jumanne juma lijalo Uingereza itakuwa ugenini kumenyana na Ukraine.

Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amesema kuwa kikosi chake hakiwezi kuidharau Moldova na wanahitaji kucheza kwa makini wakiwa na mchuano w ajuma lijalo akilini.