KENYA-SOKA

Kenya yazindua chama cha kusaidia ustawi wa wanasoka

Chama cha Ustawi wa wanakandanda nchini Kenya kinazinduliwa rasmi leo ambapo kinatarajiwa kushughulikia masuala yahusuyo wanamichezo hususan wa mpira wa miguu.

RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Akitoa wito wa kuwataka wanakandanda wote nchini humo kujiunga,mwenyekiti wa chama hicho Nicolaus Muyoti amesema kuwa wanamichezo wote wajiunge na kukitumia chama hicho kama sauti ya pamoja ya kushughulikia masuala nyeti.

Chama hicho kinachojulikana kama Kenya Footballers Welfare Association (KEFWA) kiliundwa miezi kadhaa na kusajiliwa chini ya sheria ya jamii ya mwaka 1968 na kupewa kibali cha kufanya shughuli zake na kubainisha wazi malengo yake.

Chama cha KEFWA kitajishughulisha na migogoro ya mikataba,mishahara isiyolipwa,malipo pungufu au kipato kidogo cha wachezaji,masuala ya Bima vyote vikiwa na lengo la kuhakikisha changamoto za wacheza mpira nchini humo zinahsughulikiwa na chombo maalum.

Wanamichezo wanatarajiwa kufika katika Uzinduzi huo unaofanyika jijini Nairobi katika hotel ya Indaa Park.