US OPEN -MAREKANI

Stanislas Wawrinka amng'oa Andy Murry US Open 2013

Mcheza Tennis Andy Murray amepoteza kofia ya ubingwa wa US Open katika mchezo huo baada ya kukubali kuupoteza ubingwa huo hiyo jana mikononi mwa kijana raia wa Uswizi anayekuja kwa kasi Stan Wawrinka.

REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Murray alipokutana na vyombo vya habari alikiri mchezo ulikuwa mgumu na kujikuta akiangukia pua safari hii katika michuano ya wazi nchini Marekani ijulikanayo kama US Open 2013.

Mara zote Murray amekuwa akijituma vilivyo ili kushinda katika michuano hiyo tangu michuano ya Wimbledon ya miezi miwili iliyopita.

Murray hakujaribu kujitetea kufuatia kubwagwa na Wrawinka ambapo alimsifia mpinzani wake huyo kwa kufanya mashambulizi yaliyomtoa kwa kipigo cha seti 6-4,6-3,6-2.