MAREKANI

Costa Rica yailaza Marekani 3-1 michuano ya CONCAF

Baadhi ya wachezaji wa Costa Rica wakifurahia ushindi
Baadhi ya wachezaji wa Costa Rica wakifurahia ushindi yanksarecoming.com

Timu ya Costa Rica imefifisha mbio za Marekani kuelekea katika kombe la dunia mwaka 2014 kwa kuipa kichapo cha magoli 3-1 jana Ijumaa, wakati Mexico imeshuhudia mzizimo wa hali ya juu baada ya kupoteza nafasi kwa kuchapwa magoli 2-1 na Honduras. 

Matangazo ya kibiashara

Costa Rica imesogea katika nafasi ya juu kwenye kundi la mataifa sita yaliyofuzu michuano hiyo ya CONCAF ikiibuka na ushindi huko San Jose kwenye mtanange uliotamatisha mechi ya 12 ushindi mwembamba wa Marekani .

Timu hiyo kwa sasa inaongoza kundi hilo kwa alama 14 , ikiizidi timu ya taifa ya Marekani kwa alama moja.

Mexico, ambao wamekuwa vinara wa muda mrefu katika kanda hiyo, wako katika hali mbaya zaidi wakati wakielekea katika duru nyingine muhimu ya mechi ya Jumanne.