ITALIA GRAND PRIX

Hamilton: Sijakata tamaa kuwania taji la ubingwa wa dunia wa mbio za langalanga

Dereva wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton ambaye mwishoni mwa juma ameshuhudia akimaliza kwenye nafasi ya 9 wakati wa mbio za Italia Grand Prix, amesema hakatishwi tamaa na matokeo ya siku ya Jumapili.

Dereva wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton
Dereva wa kampuni ya Mercedes, Lewis Hamilton Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo, Hamiliton amesema kuwa anafahamu changamoto iliyoko mebele yake lakini hajakata tamaa kwenye mbio za kuwania taji la dunia kati yake yeye, Sebastian Vettel wa kamouni ya Redbull na Fernando Alonso wa kampuni ya Ferrari.

Kwenye msimamo wa kinyan'ganyiri hicho, dereva Sebastina Vettel anaongoza kimsimamo akiwa na alama 222, akifuatiwa kwa ukaribu na Fernando Alonso mwenye alama 169 huku Hamilton akishika nafasi ya tatu akiwa na alama 141.

Kwa ushindi alioupata Vettel hiyo jana umekuwa ni ushindi wake wa 6 kwa mwaka huu akimuacha hamilton kwa alama 81 zaidi.

Kwenye mbio za Italia, Sebastian Vettel aliibuka mshindi huku nafasi ya pili ikishikwa na Fernando Alonso, nafasi ya tatu ikashikiliwa na Mark Webber toka Red Bull, huku nafasi ya nne ikishikwa na Felipe Massa toka kampuni ya Ferrari na Nico Hulkenberg wa Sauber akishika nafasi ya tano.

Nafasi ya sita ilishikiliwa na dereva Nico Rosberg wa Mercedes, hukiu nafasi ya saba ikienda kwa Daniel Ricciardo wa Toro Rosso, nafasi ya nane ikaenda kwa Romain Grosjean wa Lotus, nafasi ya Tisa ikashikwa na Lewis Hamilton huku nafasi ya kumi ikikamatwa na Jenson Button wa McLaren.