UEFA WORLD CUP QUALIFICATIONS

Timu ya taifa ya Uingereza kwenye mtihani mwingine wa kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia nchini Brazil

Miamba mbalimbali ya soka barani Ulaya hasa timu za taifa, hii leo zitajitupa viwanjani kumenyana katika muchuano ya kuwania kukata tiketi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia hapo mwakani nchini Brazil. 

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, John Terry ambaye leo ataiongoza timu yake dhidi ya Ukraine
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, John Terry ambaye leo ataiongoza timu yake dhidi ya Ukraine Reuters
Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Uingereza ambayo iko kwenye kundi H itakuwa ugenini mjini Kiev nchini Ukraine kupepetana na timu ya taifa ya nchi hiyo kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa kipimo kwa kocha Roy Hodgso.

Kwenye mechi hiyo nahodha msaidizi Frank Lampard anatarajiwa kuichezea timu ya taifa lake mechi ya 100 na kuungana na wachezaji wengine kama David Beckham na Steven Gerald ambao nao wameichezea timu hiyo mechi zaidi ya 100.

Mechi nyingine kwenye kundi hilo, San Marino watakuwa wenyeji wa Poland kwenye mechi nyingine ambayo inatarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Mechi nyingine ambazo zinavuta hisia za mashabiki wa soka kwenye bara la Ulaya ni zile za kundi D ambapo timu ya taifa ya Romania itakuwa na kibarua dhidi ya Uturuki, wakati Hungary watakuwa wenyeji wa Estonia, huku Andorra wakiwakaribisha Uholanzi.

Mechi nyingine ni za kundi C, ambapo timu ya taifa ya Kazakhstan itakuwa wenyeji wa
Sweden, wakati timu ya taifa ya visiwa vya Faroe watakuwa wenyeji wa Germany, mechi nyingine itawakutanisha timu ya taifa ya Austria watakaokuwa wenyeji wa Ireland.