Raikkonen kuziba nafasi ya Felipe Massa kwenye kampuni ya Ferrari
Dereva wa magari yaendayo kasi zaidi duniani maarufu kama langalanga ama Formular one, Kimi Raikkonen anatarajiwa kurejea kwenye timu yake ya zamani wa Ferrari baada ya kuihama timu hiyo mwaka 2007.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Taarifa za Raikkonen kutaka kujiunga na timu Ferrari kwenye msimu wa mwaka 2014 zinakuja wakati huu ambapo dereva wa kampuni hiyo Felipe Massa akitangaza kuachana na timu hiyo mara baada ya msimu wa mwaka 2013 kumalizika.
Massa ametangaza hatua yake ya kuihama timu ya Ferrari ifikapo mwishoni mwa msimu huu kwenye mtandao wake wa Twitter na kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano ambao wamemuonesha.
Kuondoka kwa Massa kwenye timu ya Ferrari kunaelezwa na wachambuzi wa mambo kuwa huenda kumetokana na kuhitilafiana na uongozi wake na hata dereva mwenzake Fernando Alonso hali inayomfanya ashindwe kufanya mizuri kwenye mashindano ya mwaka.
Iwapo dereva Raikkonen atajiunga na timu ya Ferrari atakuwa mmoja kati ya madereva ambo wanaenda kuunda timu ya kipekee kwenye kampuni ya Ferrari ambayo kwa siku za hivi karibuni imekuwa haifanyi vizuri.
Taarifa za siri zinasema kuwa tayari dereva huyo ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia kampuni ya Ferrari ingawa kampuni hiyo haijathibitisha.