MPIRA WA MIGUU

Trapattoni abwaga manyanga kuifundisha timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland

Kocha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Giovanni Trapattoni ametangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo kwa makubaliano maalumu baada ya kushuhudia timu yake ikipoteza mchezi wa siku ya Jumanne dhidi ya Austria.

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland
Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Trapattoni kutangaza kujiuzulu kuifundisha timu hiyo kunaelezwa na wachambuzi wa mambo kuchangiwa na sababu nyingi ikiwemo ya kushindwa kupata ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Austria kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia nchini Brazil hapo mwakani.

Jamhuri ya Ireland ilikubali kufungwa bao moja kwa ngune na timu ya taifa ya Austria na kuiweka pabaya zaidi timu hiyo katika kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwakuwa sasa inasubiri tu miujiza ya kimahesabu kwenye kundi lake ili iweze kufuzu.

Ili timu hiyo iweze kusonga mbele na kukata tiketi ya kufuzu kucheza fainali hizo italazimika kushinda mchezo wake dhidi ya timu ya taifa ya Sweden ambapo ikishinda itafanikiwa kuchupa mpaka kwenye nafasi ya pili ya kundi C.

Trapattoni amewashukuru mashabiki wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland kwa kumuonesha ushirikiano kwa kipindi chote ambacho amekuwa na timu hiyo, ambapo mwaka 2012 alifanikisha timu hiyo kucheza fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya.

Taarifa ya kujiuzulu kwa Trapattoni ilitangaza na uongozi wa chama cha soka nchini humo, ambapo kimesema baada ya mazungumzo na kocha huyo pamoja na msaidizi wake Marco Tardelli wamekubaliana kimsingi na kukubali kumuachia kocha huyo.

Mkataba wa kocha huyo ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka 2014.