AFRICA WORLD CUP QUALIFICATION

FIFA yakataa rufaa ya Congo, yaiondoa Cape Verde kushiriki hatua ya mtoano, Tunisia yarejeshwa

Wachezaji wa timu ya taifa ya Cape Verde wakiimba wimbo wa taifa kwenye moja ya mashindano, timu yao imeondolewa kushiriki hatua ya mtoano kucheza fainali za kombe la dunian 2014
Wachezaji wa timu ya taifa ya Cape Verde wakiimba wimbo wa taifa kwenye moja ya mashindano, timu yao imeondolewa kushiriki hatua ya mtoano kucheza fainali za kombe la dunian 2014 Reuters

Shirikisho la kabumbu duniani FIFA limeiondoa nchi ya Cape Verde kucheza haua ya mtoano kuwania kucheza fainali za kombe la dunia baada kumchezesha mchezaji aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye ripoti yake FIFA imesema kuwa Cape Verde ilimchezesha kimakosa mchezaji, Fernando Verela kimakosa sababu alikuwa akitumia adhabu ya kutocheza mechi nne badala ya tatu kama sheria inavyotaka.

nchi ya Tunisia ilikata rufaa kupinga mchezaji huyo kucheza kwenye mechi yao ambayo ilishuhudiwa Tunisia wakikubalia kichapo cha mabao 2-0 kwa nunge na hivyo kutupwa nje kwenye kinyan'ganyiro hicho.

Kwenye uamuzi wake pia FIFA imekipiga faini chama cha soka nchini Cape Verde na kuitaka ilipe kiasi cha dola elfu 4 na 300 kama adhabu ya kumtumia mchezaji huyo kimakosa.

Tunisia sasa imezawadia ushindi wa mabo 3-0 pamoja na alama tatu na sasa itajumuishwa kwenye hatua ya makundi ya mtoano kuwania nafasi tano za kwenda nchini Brazil kushiriki fainali za kombe la dunia.

Katika hatua nyingine, FIFA pia imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na shirikisho la soka la Congo lililotaka ufafanuzi kuhusu nchi ya Niger kumchezesha mchezaji, Mahamane Cisse ambaye kipindi fulani alichezea nchi ya Mali.

Congo inadai kuwa mchezaji huyo ni halali kuchezea nchi ya Mali na sio NIger kama alivyochezeshwa kwenye mechi ya juma lililopita ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 na hivyo kuinyima kongo nafasi ya kusonga mbele.

Kwa uamuzi huo sasa Burkina Faso ndio timu iliyofanikiwa kutinga hatua ya mtoano kuwania kukata tiketi ya kwenda nchini Brazil kucheza fainali hizo.

Kwenye taarifa yake FIFA imeridhishwa na hatua ya mchezaji huyo kuamua kubadili uraia wake na na kuchezea nchi ya Niger.