TUNISIA-SOKA

Tunisia yatangaza kocha wa mpito kwa ajili ya maandalizi ya kufuzu kwa kombe la dunia

Shirikisho la soka nchini Tunisia limemtangaza Ruud Kroll kuwa kocha wa mpito wa kikosi cha Taifa kinachojiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014. Kroll anaziba pengo lililoachwa na Kocha Nabil Maaloul aliyejizulu baada ya kichapo cha nyumbani cha mabao 2-0 toka kwa Cape Verde Septemba 7 mwaka huu.

http://www.supersport.com
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa Kroll anainoa klabu ya CS Sfaxien na ataendelea kutimiza majukumu yake yote kwa klabu hiyo na kwa timu ya Taifa.

Rais wa SC Sfaxien Lotfi Abdennadher na Rais wa Shirikisho la soka la Tunisia Wasii Al Jarii wamekubaliana kuwa kocha huyo atakiongoza kikosi hicho katika mzunguko wa mwisho mechi za mataifa ya Afrika yaliyosalia katika orodha ya kuwania kufuzu kwa kombe la dunia.

Kwa mujibu wa Shirikisho hilo, Krull ataiongoza Tunisia iliyojipatia nafasi baada ya Cape Verde kubanduliwa nje kwa kosa la kumshirikisha mchezaji aliyekuwa amepigwa marufuku katika mechi yao dhidi ya Tunisia Jumamosi iliyopita.

Uamuzi wa Rufaa uliotolewa na Shirikisho la soka duniani FIFA ulibaini kuwa mchezaji Fernando Verela hakufaa kucheza katika mechi hiyo na uamuzi huo umeipa Tunisia ushindi mkubwa wa mabao 3-0 .