MICHEZO

Mfaransa Sebastien Ogier ashinda mbio za Australia

Mfaransa Sebastien Ogier ameshinda mbio za magari za Australia leo Jumapili lakini msukumo wake kwa ubingwa wa mbio za magari za dunia FIA umeendelea kushikiliwa hadi ligi ijayo nchini Ufaransa mwezi ujao.

Sebastien Ogier
Sebastien Ogier ausmotive.com
Matangazo ya kibiashara

Dereva huyo wa Volkswagen ameshinda hatua 17 kati ya 22, ikiwa ni pamoja na hatua ya nguvu, na kumaliza kwa muda wa dakika moja na sekunde 32 Mbele ya Thierry Neuville wa Ubelgiji.

Naye Dereva Mikko Hirvonen kutoka Finland amemaliza mbio hizo akishika nafasi ya tatu katika muda dakika 02na sekunde 1 nyuma ya mshindi.

Lakini ilikuwa ni bahati mbaya kwa upande wa Hirvonen katika umbali wa kilomita 29.44 kupita katika hatua ya Shipmans karibu na ufukwe wa Coofs kaskazini mwa New South Wales ambayo ilisabaisha kupoteza matumaini ya kupata ubingwa wa Ogier