RONALDO-REAL MADRID

Ronaldo aongeza mkataba na klabu yake ya Real Madrid, anakuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani

Mshambuliaji wa timua ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo
Mshambuliaji wa timua ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo REUTERS/Ina Fassbender

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania, Christian Ronaldo hii leo ameongeza mkataba mwingine wa kuitumikia klabu hiyo mpaka kufikia mwaka 2018 huku akiwa ni mchezaji anayelipwa ghali zaidi duniani.

Matangazo ya kibiashara

Kuongeza mkataba kwa mshambuliaji huyu kunakuja kufuatia uvumi uliokuwepo hapo awali kuwa nguli huyo angeihama klabu hiyo na kujiunga na klabu za nchini Ufaransa ambazo zilionesha nia ya kumnasa mchezaji huyo.

Christian Ronaldo ameongeza mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu yake ya Real Madrid mkataba ambao unamaanisha kuwa mshambuliaji huyo huenda akamalizia soka lake klabu hapo.

Mchezaji huyu anatarajiwa kupokea mshahara wa kiasi cha Euro milioni 20 kwa msimu na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa ghali zaidi duniani akifuatiwa na mpinzani wake anayekipiga klaby ya FC Barcelona, Lionel Messi anayelipwa Euro milioni 16 kwa msimu.

Ronaldo ambaye uhamisho wake ulivunja rekodi ya dunia wakati alipojiunga na timu hiyo akitokea Manchester United ya nchini Uingereza kwa dau la Euro milioni 90 mwaka 2009 ambapo amefanikiwa kufunga mabao 203 kwenye mechi 203 alizocheza.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari wakati akitangaza kumuongezea mkataba mchezaji huyo, rais wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kuwa wanajivunia kuwa na mchezaji mwenye kiwango kama Chrisian Ronaldo na wanafuraha kumbakiza mchezaji huyo.