Michezo

Ligi ya mabingwa barani Ulaya kutimuwa vumbi hii leo

Michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya
Michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya

Ligi ya mabingwa barani Ulaya inatimua vumbi leo usiku katika vinwanja tofauti ambapo Manchester United watakuwa na Bayern liverkusen ya Ujerumani ambapo kila timu inataraji kuonyesha Ushindani mkubwa katika mpambano huo wa kukata na shoka. 

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji waliosajiliwa katika msimu huu kuvuchezea vilabu mbalimbali barani ulaya wanataraji kuonyesha mchezo mzuri katika mechi zinazo tarajiwa kupigwa jioni hii. Kocha wa Machester United David Moyes amesema amewapanga wachezaji wake vizuri na mchezo ni mchezo anataraji matokeo mazuri.

wakati huo huo Real Madrid watakuwa uwanjani kuchuana na Galatasaray, ambapo mchezaji nyota Gareth Bales aliesajiliwa kutoka Uingereza katika Klabu ya Tottenham anataraji kuonyesha kwamba kocha wa Real Madrid hakukosea kumsajili katika Klabnu hiyo. Mechi hii, inataraji kushuhudiwa ushindani mkubwa ambapo Klabu ya Galatasaray anayoichezea Didier Drogba mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye pia anataraji kuonyesha kwamba bado anauwezo wa kuhimili mikiki ya michuano hiyo.

Mechi nyingine ambazo zitashuhdiwa usiku huu ni pamoja na Bayern Munich itayo chuana na CSKA Mosco, Victoria Pizen itakuwa dimbani kumenyana na Manchester City, Real Sociedad itapepetana na Shaktar Donesk, FC Copenhagen itamenyana na Juventus FC, Olympiakos itapambana na Paris Saint Germain, Benfica itakuwa uwanjani kuchuana na Anderlech ya Ubelgiji