FOOTBALL-MANCHESTER UNITED

Wayne Rooney aandika bao la 200 akiwa na klabu ya mashetani wekundu

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ambae alitajwa kuwa ataondoka msimu wa baridi uliopita Wayne Rooney mwenye umri wa miaka 27 ambaye tayari amecheza mechi moja na kufunga mabao 2 katika mechi ya daraja la kwanza na ambaye aliamuwa kusalia katika klabu yake ya Manchester United.

Matangazo ya kibiashara

Hili ni moja miongoni mwa mambo yanayo mpa furaha kubwa kocha wa klabu hiyo David Moyes na mashabiki wa Klabu hiyo.

Ronney alifaulu kupachika nyavuni mabao 2 katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya iliopigwa jana wakati wa mpambano wao na Bayern Leverkusen na kuandika historia ya kutimiza mabao 200 akiwa na klabu hiyo ya mashetani wekundu.

Wachezaji watatu pekee ndio ambao wanarikodi hiyo katika klabu hiyo ikiwa ni pamoja na Jack Rowley alitimiza mabao 211 Denis Law mabao 237 pamoja na Bobby Charlton aliefikisha mabao 249.

wakati huo huo mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo Robert Van Persie amesema anafurahia sana kucheza pamoja na Rooney kwa kuwa anajuwa kusaka mpira na unauwezo wa kucheza mipira mifupi na mirefu.
Matamshi ambayo yamempa matumaini makubwa kocha wa Manchester Unites David Moyes.