Football-ligi ya mabingwa

Arsenal, Barcelona, Chalke 04 zatamba, chelsea, Marseille za tota

Klabu ya Arsenal imeanza vizuri Ligi ya Mabingwa baranai Ulaya baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Marseille katika Uwanja wa Velodrome, nchini Ufaransa. Mabao ya Gunners yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 65 na Aaron Ramsey dakika ya 83, wakati la wenyeji lilifungwa na Jordan Ayew kwa penalti dakikakwenye dakika ya 90.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Klabu ya Barcelona ilikuwa uwanjani kumenyana na Ajax ambapo mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi amefunga mabao matatu katika ushindi huo wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, mechi iliopigwa kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Lionel Messi mbali na kufunga mabo hayo matatu peke yake jana usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique. Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson. Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.

katika hatuwa nyingine, Jose Mourinho amepata kipigo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-1 nyumbani na FC Basle.

Oscar alitangulia kuwafungia The Blues dakika ya 45, lakini Salah akasawazisha dakika ya 71, kabla ya Streller kufunga la ushindi dakika ya 82 Uwanja wa Stamford Bridge.

Nayo klabu ya Chalke 04 iliifunza kandanda klabu ya Steaua Bucarest kwa kuicharaza mabao 4-0, maboa ambayo yalipachikwa nyavuni na Uchida 67’ Boateng 78’ Draxler 85’.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, AC Milan iliichapa Celtic 2-0 Uwanja wa San Siro, mabao ya Zapata dakika ya 82 na Muntari dakika ya 85.