Michezo-Football

Real Madrid yailaza Getafe mabao 4-1

Klabu ya Real Madrid ya huko Uhispania imeilaza klabu ya Getafe kwa mabao 4 – 1 ikiwa ni michuano ya ligi kuu nchini humo.Timu hiyo ilianza vibaya mchezo hio kwanza mchezaji Gareth bales alijeruhiwa wakati akifanya mazoezi ya kupasha mwili moto kabla ya kuanza kwa mchezo, na katika dakika tano za mchezo mshambuliaji Angel Lafita aliliona lango la Real na kuandika bao la kwanza.

Real Madrid yailaza Getafe FC kwa mabao 4-1
Real Madrid yailaza Getafe FC kwa mabao 4-1 www.google.co.
Matangazo ya kibiashara

Real Madrid wakiwa nyumbani walitakiwa kuonyesha uwezo na kusawasizisha katika dakika ya 19 na mchezaji Pepe, huku Christiano Ronaldo akipachika mawili na kuandikisha bao la 208 na 209 katika klabu hiyo na kumshinda Hugo Sanchez ambaye anachukuwa nafasi ya tano katika wafungaji wa mabao mengi katika klabu hiyo.

Mshambuliaji Isco ndiye aliye pachika bao la 4 la Real Madrid na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kulala roho baridi.

Katika matukio mengine FC Betis Séville ilitoka sare ya bila kufungana na Granada FC. Valence ikaitandika FC Seville mabao matatu kwa moja, huku Celta Vigo na Cillarreal zikashindwa kufungana na kulazimishana sare ya 0-0.