Tennis

Venus Williams atinga nusu fainali za Pan Pacific Open

Mcheza Tennis Venus Williams amemchakaza Eugenie Bouchard wa Canada kwa seti tatu za 6-3, 6-7 na 6-3 leo Alhamisi na hivyo kujikatia tiketi ya kushiriki nusu fainali ya mashindano ya Pan Pacific Open. 

Venus Williams
Venus Williams cbc.ca
Matangazo ya kibiashara

Williams,ambaye anashiriki mashindano ya Tokyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006, amefanikiwa kumdhibiti mdhibiti Bourchard katika seti ya tatu na kushikilia ushindi wa mechi hiyo ambayo imemalizika kwa saa tatu na dakika mbili huko Ariake.

Williams atakutana na Svetlana Kuznetsova aua Petra Kvitova katika nusu fainali zijazo.

Kvitova raia wa Jamhuri ya Czech alimshinda Madison Keys wa Marekani kwa seti mbili za 6-2, 6-2 wakati Kuznetsova wa Urusi alimchakaza Sorana Cirstea wa Romania kwa seti nne za 7-6 (3),6-1