Football-Arsenal

Mmiliki wa klabu ya Arsenal Stan Kroenke ataka Wenger abaki kwenye klabu hiyo

Mmiliki wa klabu ya Arsenal, Stan Kroenke
Mmiliki wa klabu ya Arsenal, Stan Kroenke arsenalarsenal.wordpress.com

Mmiliki wa klabu ya Arsenal, Stan Kroenke ameweka bayana kuwa anataka meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger aendelee kukaa katika klabu hiyo na kukomesha ukame wa ushindi kwa timu hiyo al maarufu the Gunners. 

Matangazo ya kibiashara

Wenger amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 17 lakini timu hiyo kwa sasa imeingia katika msimu wake wa tisa bila kupata taji lolote , taji lao la mwisho likiwa la mwaka 2005 la kombe la FA.

Mkataba wa Wenger uko mbioni kumalizika baada ya kutamatika kwa kampeni za sasa na kumekuwa na uvumi kuhusu mkataba wa muda mrefu kwa bosi huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 63.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo raia wa Marekani Kroenke, katika mahojiano adimu hii leo na gazeti la Daily Telegraph, ameweka wazi kuwa anataka Wenger aendelee kuitumikia klabu hiyo kwa kuwa hana mtu mwingine anaye mwamini kwa kazi nzuri kama Wenger.

Akizungumzia kauli ya Kroenke,Wenger amesema kuwa amejihisi mwenye heshima kubwa kuungwa mkono na Stan na kwamba kuutambua mchango wake katika klabu hiyo ni kura ya uaminifu kwake yenye ujazo mkubwa.

Kufuatia kupoteza mchezo katika mechi ya ufunguzi ya msimu huu kati ya Arsenal na Aston Villa ambapo arsenal ilifungwa magoli 3-1, kwa sasa timu hiyo inaongoza ligi kuu kwa tofauti ya magoli kutoka kwa wapinzani wajadi Tottenham Hotspurs kabla ya mechi ya Kesho Jumamosi dhidi ya Swansea City.