TENNIS

Petra Kvitova azima ndoto za Venus Williams mashindano ya Pan Pacific Open

Bingwa wa mashindano ya tenesi ya Wimbledon mwaka 2011 Petra Kvitova amezima ndoto za Venus Williams za kushiriki fainali za mashindano ya Pan Pacific Open leo Ijumaa, baada ya kumtandika mikwaju ya seti tatu za 3-6, 6-3, 7-6 na kufuzu kukabiliana na Angelique Kerber kuwania kitita cha dola 2,300,000 katika fainali. 

Mcheza Tenesi Petra Kvitova
Mcheza Tenesi Petra Kvitova www.zimbio.com
Matangazo ya kibiashara

Mjerumani Angelique Kerber ameonesha nguvu kubwa dhidi ya mdenimark Caroline Wozniacki kwa kumrambisha mchanga kwa kipigo cha seti mbili za 6-2, na 7-6 na hatimaye kutinga katika fainali kwa mara ya saba tangu aingie katika fani hiyo.

Kvitova, ambaye ni bingwa wa mashindano ya Wimbledon mwaka 2011 kutoka Jamhuri ya Czech, alisambaratisha mashambulizi yote yaliyoelekezwa kwake na Williams katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa huko Tokyo, na kumfanya bingwa huyo namba saba kukaza msuli wake na hatimaye kuibuka na ushindi katika mchezo saa mbili na dakika dakika 24

Kvitova amesema kuwa mchezo wa leo ni mmoja kati ya michezo bora aliyocheza msimu huu ambapo ameongeza kuwa alijua kutakuwa na mashambulizi kutoka kwa mpiznani wake na hivyo alijitahidi kushambulia kadiri alivyoweza.