SOKA-UINGEREZA

Kocha wa zamani wa Manchester United Ferguson akanusha madai ya kwamba anataka kurejea kuifunza Timu hiyo

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwasalimia mashabiki
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwasalimia mashabiki REUTERS/Phil Noble

Kocha wa zamani wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amekanusa taarifa zilizokuwa zimezagaa ya kwamba yupo mbioni kurejea tena kwenye kazi yake ya kuongoza Timu hiyo kutokana na kushuhudia matokeo mabaya kwa klabu yake ya zamani. Ferguson amesema hana mpango wala nia ya kurejea tena kuwa Kocha kwani anaamini kazi yake ameshaifanya ipasavyo na sasa ataendelea kufamnya shughuli nyingine nje ya kuwa mkufunzi.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 71 amesema hawezi akarejea tena nyuma eti kwa sababu Manchester United inashika nafasi ya kumi na mbili kwenye msimamo wa ligi kwani anaamini ipo kwenye mikono salama.

Ferguson ametumia fursa hiyo kumtetea mrithi wake David Moyes na kusema anaamini ni mkufunzi bora kabisa ambaye ayaisaidia Manchester United kuendelea kuwa timu tishio Barani Ulaya.

Mkufunzi huyo aliyejizolea umaarufu kutokana na kuipa mafanikia makubwa Manchester United baada ya kuinoa kwa karibu miaka ishirini na sita amesema anaamini Moyes atakuwa na wakati mzuri sana Old Trafford.

Kocha huyo aliyefanikiwa kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu nchini Uingereza, Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mara mbili, Kombe la Chama Cha Soka mara tano na Kombe la Ligi mara nne amesema kwa sasa anapaswa kupumzika.

Ferguson pia amefichua siri ya kwamba alitakiwa na Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich mwaka 2003 ili aweze kupewa kibarua cha kuifundisha lakini alikataa ofa hiyo nono.

Fergie kama anavyotambulika zaidi anasema alimwambia wazi Abramovich hakuna nafasi ya yeye kujiunga na Chelsea kwa kuwa alikuwa na Timu bora na yenye uchu wa kupata mafanikio.