SOKA-FIFA-UEFA-QATAR

Blatter aendelea kupata upinzani juu ya mpango wake wa kusogeza mashindano ya Kombe la Dunia majira ya joto nchini Qatar

Rais wa FIFA, Sepp Blatter akionesha bahasha iliyoipa ushindi nchi ya Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022
Rais wa FIFA, Sepp Blatter akionesha bahasha iliyoipa ushindi nchi ya Qatar kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022 Reuters

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA Sepp Blatter ameendelea kukumbana na upinzani mkali juu ya pendekezo lake la kutaka kuhamisha mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022 yaliyopangwa kufanyika nchini Qatar wakati wa majira ya baridi. Blatter amependekeza mashindano ya Kombe la Dunia yaliyopangwa kufanyika nchini Qatar kusogeza kutoka majira ya joto hadi yale ya baridi kutokana na wakati huwa joto kuwa kali mno na huenda likawathiri wachezaji.

Matangazo ya kibiashara

Upinzani wa hivi karibuni aliokutana nao Blatter unatoka kwa wajumbe watatu wa Kamati Kuu wa FIFA wanaosema hakuna umuhimu wa kusogeza mashindano hayo majira ya baridi kwani hali hiyo itachangia kubadilishwa kwa ratiba ya ligi mbalimbali.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya FIFA aliyeketaa kutajwa jina lake amesema ratiba hiyo inaweza ikabadilishwa tu iwapo wasimamizi wa Ligi na wadau watashauriwa na hatimaye kuafikiana na mpango huo utakaosababisha madhara kwa ratiba za soka.

Rais wa FIFA Blatter amekuwa akifanya kampeni ya hali ya juu kutashinikiza mabadiliko ya muda wa kufanyika kwa mashindano hayo ya nchini Qatar kwani joto linaloweza kufikia sentigredi 40 litakuwa kikwazo.

Mataifa kadhaa yameonekana kuwa tayari kuona ratiba ya Komba la Dunia inabadilika japokuwa kuna wale ambao wamekuwa akipinga hasa Klabu kubwa Barani Ulaya zinazohisi huenda zikaathirika kutokana na uamuzi huo.

Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA lenyewe limeendelea kutofautiana juu ya uamuzi huo wa kusogeza mbele mashindano hayo hadi majira ya baridi kwani wengi wanahofia madhara yatakayochangiwa na hali hiyo.

Rais wa UEFA Michel Platini anasema ni kitu kigumu sana kuamua na iwapo kura itapigwa basi kunaweza kukatokea matokeo tofauti na hivyo wakati wa mjadala upo na suala hili linafaa kuendelea kujadiliwa.