Michezo

Nusu fainali ya Michuano ya Klabu bingwa na shirikisho barani Afrika kusakatwa jumapili

Michuano ya nusu fainali ya kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika na shirikisho zinachezwa mwishoni mwa juma hili.
Michuano ya nusu fainali ya kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika na shirikisho zinachezwa mwishoni mwa juma hili. rfikiswahili

Michuano ya nusu fainali ya kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika na shirikisho zinachezwa mwishoni mwa juma hili.

Matangazo ya kibiashara

Orlamndo Pirates ya Afrika Kusini wakiwa nyumbani jana Jumamosi walitoka sare ya kutofunga na mabingwa wa mwaka wa 2011 Esperence ya Tunisia.

Matokeo haya yanamaanisha kuwa Esperence ya Tunisia wana matuamaini makubwa ya kusonga mbele kwa kutofungwa nyumbani licha ya kocha Maher Kanzari kusema kuwa hayakuwa matokeo mazuri kwa vijana wake ambao watakuwa nyumbani kuwakaribisha Orlando Pirates baada ya wiki mbili zijazo.

Naye kocha wa Orlando Pirates Roger de Sa amesema kuwa watakapokwenda nchini Tunisia itabidi watuie mbinu zote na kuibuka na ushindi.

Mchuano wa pili kati ya mabingwa wa tetezi Al Alhy ya Misri na CotonSport ya Cameron uliahirishwa na sasa utachezwa leo Jumapili mjini Garoua .

Refarii wa mchezo huo Jan Sikazwe kutoka nchini Zambia alisitisha mchuano huo wakati kabla ya timu zote kupata bao katika mchuano huo.

Sheria za shirikisho la soka barani Afrika CAF zinasema kuwa mchuano ukisimamishwa kwa sababu kama hiyo utachezwa ndani ya saa 24 katika uwanja huo na kusimamiwa na Marefarii waliocheza mchuano wa kwanza.

Katika michuano ya shirikisho CA Bizertin na CS Sfaxien zote za Tunisia zitamenyana katika nusu fainali ya kwanza, huku St Malien ya Mali ikiwa nyumbani dhidi ya TP Mazembe.

Mchambuzi wa soka wa RFI Kiswahili Kahozi Kosha akiwa mjini Lumbumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa ni muhimu kwa TP Mazembe kushinda mchuano wa jumapili ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu katika hatua ya fainali wiki mbili zijazo.

TP Mazembe haijawahi kunyakua taji katika michuano hii ya shirikisho.

Mechi za mzunguko wa pili zitachezwa baada ya wiki mbili.