SOKA-ENGLAND

Matumaini ya England kukata tiketi ya kushiriki kombe la dunia 2014 yaongezeka

http://www.dailymail.co.uk

Timu ya soka ya Uingereza na imeongeza matumaini ya kufuzu katika Kombe la Dunia baada ya kuifunga Montenegro mabao 4-1 katika mechi iliyopigwa usiku wa kuamkia leo.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Uingereza yamepachikwa na Wayne Rooney dakika ya 48, Branko Boskovic dakika ya 62, Andros Townsend dakika ya 78 na Daniel Sturridge katika dakika ya 90 kwa mkwaju wa penati.

Kocha Mkuu wa kikosi hicho Roy Hodgson amesema anatumaini ya kufanya vyema zaidi ili kukata tiketi ya kutinga katika fainali hizo na hata kutwaa ubingwa.

Kwa sasa England inasubiri kuchuana na Poland siku ya jumanne na inahitaji ushindi mwingine ili ijitwalie nafasi ya kwenda Brazili.

Ujerumani, Ubelgiji na Uswisi tayari zimekwishafuzu kutinga fainali hizo zitakazopigwa nchini Brazil mwaka ujao.

Ujerumani imepata nafasi hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jamuhuri ya Ireland katika mechi za kundi C. Mabao ya Brazil yamepachikwa kimiani na Sami Khedira, Andre Schuerrle na Mesut Ozil.

Ubelgiji imjitwalia nafasi hiyo kupitia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia na hivyo kuongoza kundi A. Mabao yote yalipachikwa kimiani na mshambuliaji wa Everton Romeu Lukaku katika dakika ya 16 na 38 ya mchezo huo.

Uswisi iliyoumana na Albania ilijipatia ushindi wa mabao 2-1na kujinyakulia nafasi ya uongozi katika kundi E. Mabao ya Xherdan Shaqiri na Michael Lang ndiyo yaliyoipa ushindi Uswisi katika mechi hiyo.

Mataifa hayo yanaungana na Italia na Nertherland ambao tayari waliishajipatia tiketi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2014.