michezo

Dereva wa mbio za magari Sean Edwards aafariki katika ajali Australia

Sean Edwards dereva raia wa Uingereza ameaga dunia baada ya kupata ajali
Sean Edwards dereva raia wa Uingereza ameaga dunia baada ya kupata ajali RFI

Dereva wa mbio za magari ambaye anashiriki vema katika mchezo huo Sean Edwards amefariki dunia katika mchezo huo baada ya kugongana huko Queensland nchini Australia.

Matangazo ya kibiashara

Muingereza huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 26 alikuwa ndani ya gari kama abiria wakati madereva wachanga walipokuwa katika jaribio binafsi.

Edwards kwa siku za hivi karibuni ndiye amekuwa akiongoza ubingwa wa mchezo huo awamu ambazo zinaenda sambamba na mbio za magari za Formula 1.

Edwards ambaye ni mtoto wa mwanamichezo wa siku nyingi alikuwa akishiriki katika siku ya pili ya uangalizi kwa madereva wachanga huko Queensland ambapo aliyekuwa akiendesha gari amejeruhiwa.

Kwa sasa kijana huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ambapo bado ana maumivu katika majeraha.