SOKA

Orodha ya wachezaji wanaowania taji la mchezaji bora dunia yatolewa

DR

Mchezaji wa soka Gareth Bale aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa cha fedha duniani msimu huu ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa katika orodha ya wachezaji 23 wanaowania kuwa mchezaji bora mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Bale ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid ya Uhispania anaungana na wachezaji wengine watano kutoka ligi kuu ya soka nchini Uingereza kama vile Eden Hazard, Mesut Ozil, Luis Suarez, Yaya Toure na Robin van Persie ambao pia wamejumuishwa katika orodha hiyo.

Naye mshambulizi wa Kimataifa wa Barcelona Lionel Messi atakuwa anawania kulihifadhi taji hilo ambalo amekuwa akilishinda kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Messi atapambana na wachezaji wenzake kama Andres Iniesta, Neymar, na Xavi pamoja na mpinzani wa siku nyingi Cristiano Ronaldo ya Real Madrid.

Wayne Rooney wa Manchester United ambaye alijumuishwa katika orodha ya mwaka uliopita hakupata nafasi hiyo mwaka huu, huku kukiwa hakuna mchezaji yeyote aliyesajiliwa kutoka Uingereza, Scotland na Ireland Kaskazini.

Bayern Munich ambayo iliishinda Barcelona katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya msimu uliopita imetoa orodha ya wachezaji sita wamejumuishwa katika orodha hiyo.

Hii ni ndio orodha kamili ya wachezaji wanaowania taji hilo, Gareth Bale (Real Madrid), Edinson Cavani (Paris St-Germain), Radamel Falcao (Monaco), Eden Hazard (Chelsea), Zlatan Ibrahimovic (Paris St-Germain), Andres Iniesta (Barcelona), Philipp Lahm (Bayern Munich).

Robert Lewandowski (Borussia Dortmund), Lionel Messi (Barcelona), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Mesut Ozil (Arsenal), Andrea Pirlo (Juventus), Franck Ribery (Bayern Munich), Arjen Robben (Bayern Munich), Cristiano Ronaldo (Real Madrid).

Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich), Luis Suarez (Liverpool), Thiago Silva (Paris St-Germain), Yaya Toure (Manchester City), Robin Van Persie (Manchester United), Xavi (Barcelona).

Mbali na wachezaji pia orodha ya makocha kumi bora imetolewa, miongoni mwa makocha hao ni pamoja na aliyekuwa Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson, Arsene Wenger wa Arsenal na Jose Mourinho wa Chelsea.

Wengine ni pamoja na Carlo Ancelotti (Real Madrid CF), Rafael Benítez (Napoli), Antonio Conte (Juventus), Vicente Del Bosque (Spain), Sir Alex Ferguson (Aliyekuwa kocha Manchester United).

Jupp Heynckes (Aliyekuwa kocha Bayern Munich), Jurgen Klopp (Borussia Dortmund), Jose Mourinho (Chelsea), Luiz Felipe Scolari (Brazil), Arsene Wenger (Arsenal).

Washindi watatangazwa tarehe 13 mwezi Januari mwaka ujao mjini Zurich nchini Swizerland.