Soka-Arsenal

Arsenal yazidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza

Klabu ya soka ya Arsenal imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuitandika Liverpool mabao 2-0 kwenye mechi yao ya jumamosi iliyopigwa katika dimba la Emirates jijini London.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Arsenal yalipachikwa na Santi Cazorla dakika ya 19 na la pili lilitoka kwa Aaron Ramsey dakika ya 59.

Kwa matokeo hayo Arsenal inayonolewa na kocha Arsene Wenger imejikusanyia jumla ya pointi 25 mpaka sasa baada ya kucheza michezo 10.

Liverpool inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 20 sawa za Chelsea, ambayo ilipata kichapo cha 2-0 toka kwa Newcastle.

Kwa upande wao mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu Manchester United waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham, mabao hayo yalipachikwa na Antonio Valencia, Robin van Persie and Wayne Rooney.