MESSI-BARCELONA

Messi kuwa nje ya uwanja kwa majuma 6 hadi 8

Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi ambaye klabu yake hii leo imesema atakuwa nje kwa majuma 6 hadi 8 kutokana na majeraha
Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi ambaye klabu yake hii leo imesema atakuwa nje kwa majuma 6 hadi 8 kutokana na majeraha Reuters

Klabu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania imetangaza kuwa itamkosa mchezaji wake Lionel Messi kwa zaidi ya majuma 6 hadi 8 kufuatia kuumia kwenye mchezo wao dhidi ya Real Betis siku ya Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa klabu hiyo, imesema kuwa Messi aliumia msuli wa baja wakati wa mtanange wao na Real Betis na kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa majuma sita hadi nane mpaka atakapopata nafuu.

Messi alilazimika kutolewa nje katika dakika ya 20 ya mchezo baada ya kuanguka na kuanguka na kushindwa kuendelea na mchezo kabla ya madaktari wa timu hiyo kuthibitisha kuwa hatoweza kuendelea na mechi.

Mchezaji huyo ambaye ametwaa taji la mwanasoka bora wa dunia mara nne mfululizo hii inakuwa ni mara yake ya tatu kwenye msimu huu kupata maumivu ambayo yanamfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi.

Kwenye mechi hiyo Messi alichangia ushindi wa timu yake wa mabao 4-1 dhidi ya Real Betis na kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kung'ang'ania usukani la ligi kuu ya nchini Uhispania.