LIGI KUU YA UINGEREZA

Van Persie apelekea kilio kwa mashabiki wa Arsenal, Tottenham yalala nyumbani dhidi ya Newcastle

Mshambuliaji wa Manchester United, Robin Van Persie akishangilia bao alilofunga dhidi ya Arsenal
Mshambuliaji wa Manchester United, Robin Van Persie akishangilia bao alilofunga dhidi ya Arsenal Reuters

Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger akiri wachezaji wake kucheza chini ya kiwango na uwonga kufuatia kuishuhudia timu yake ikipoteza mchezo wake ugenini kwenye uwanja wa Old Trafford dhidi ya Manchester United.

Matangazo ya kibiashara

Goli la dakika ya 27 ya mchezo lililofungwa na Robin Van Persie lilitosha kuzamisha jahazi la mashabiki wa Arsenal waliokuwa wakiamini kuwa huenda wangeifunga Man utd kutokana na siku za hivi karibuni timu hiyo kutofanya vizuri.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, alifunga bao lake kwa njia ya kichwa kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Wyne Rooney na kuamsha shamrashamra kwenye uwanja wa OT.

Bao hilo lilidumu haki kipindi cha kwanza kimalizika, ambapo kwenye kipindi cha pili klabu ya Arsenal ilikuja juu kutaka kurejesha goli hilo lakini hata hivyo ngome ya Man utd ilikuwa imara kuweza kulinda lango lao.

Katika mechi nyingine za ligi kuu ya Uingereza, timu ya Tottenhama Hotspurs wakiwa nyumbani walipoteza mchezo wao dhidi ya timu ya Newcastle baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Sunderland wenyewe wameanza kuonesha makucha yao baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Manchester City kwenye mchezo ambao hakuna aliyetarajia kuona Man City ikipoteza mchezo huo.

Swansea wakiwa nyumbani walilazimika kufanya kazi ya ziada kuwadhibiti vijana wa Stoke City ambao walianza kwa kuongoza kwa magoli mawili kabla ya Swansea kurejeasha mabao hayo na kisha kuongeza na kushuhudia mchezo huo ukimalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Msimamo wa ligi unaonesha kuwa Arsenal wanaendelea kuongoza kwa alama 25, wakifuatiwa na Liverpool yenye alama 23, Southampton yenye alama 22, Chelsea yenye alama 21 na Manchester United yenye alama 20.