SOKA-UFARANSA

Ufaransa yanyakua tiketi kushiriki kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili

Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amepongeza wachezaji wake kwa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Ukraine uliowawezesha kufuzu kushiriki kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazili. Mabao ya Ufaransa yalipachikwa kimiani na Oleg Gusev, Mamadou Sakho na Karim Benzema.

RFI/Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Deschamps amesema ulikuwa ni mchezo wa maajabu kwani siku nnne zilizopita walikuwa katiika hali mbaya baada ya kupata kichapo cha magoli 2-0 toka kwa Ukraine katika mechi yao ya awali.

Ukraine ilimaliza mechi hiyo ikiwa na wachezaji 10 baada ya Yevhen Khacheridi kuzawadiwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili cha mtanange huo.

Ukraine imepoteza nafasi ya kushiriki kombe hilo kwa mara ya nne, miaka mingine iliyopoteza nafasi hiyo ni 1998, 2002 na 2010.

Kwa upande wake kocha wa Ukraine, Mikhail Fomenko amesema kulikuwa na nafasi za wazi wachezaji wake na kabla ya kuanza mchezo huo aliwaonya kutoacha nafasi jambo ambalo anaona hawakulizingatia.