Michezo-Football

Dan Sserunkuma awasilisha ombi la uhamisho Gor Mahia

Dan Sserunkuma, amewasilisha ombi la uhamisho kwa Gor Mahia
Dan Sserunkuma, amewasilisha ombi la uhamisho kwa Gor Mahia GorMahia.net

Mwenyekiti wa Gor Mahia, Ambrose Rachier, amedhibitisha kwamba mshambuliaji matata wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Kenya, Dan Sserunkuma, anayetaka kuondoka, amewasilisha ombi la uhamisho.

Matangazo ya kibiashara

Rachier aliongeza kwamba hawana dhamira ya kukatalia mshambuliaji wao matata ila yule anayetaka huduma zake ni lazima azungumze na Gor moja kwa moja ili wakamilishe shughuli hiyo kwa haraka.

Rachier amesema alipata barua pepe kutoka Sserunkuma mnamo tarehe 15 Novemba ambapo alieleza kusudi yake kutoshiriki Ligi Kuu Kenya au Ligi ya Mabingwa ya Afrika kwani vilabu kadhaa kutoka Armenia vinataka huduma zake.

Ameeleza kuwa hakuna pingamizi lolote kwa Sserunkuma kuondoka lakini kile ametoa wito kwa timu zinazo mtaka mshambuliaji huyo ziongee na Gor ana kwa ana.

Kama ni mkopo wanatakata, waelezee matakwa yao na kama ni mkataba wa kudumu, ili makubaliano yafikiwe kama ni ada ya uhamisho ili Gor imwachilie mara moja.

Ameongeza kuwa anapaswa kutuma majina ya wachezaji watakaowakilisha kwenye Ligi ya Mabingwa kabla ya Desemba 28 na Sserunkuma ana hadi Desemba 15 kutoa musimamo wake.

Aidha Gor Mahia ililipa City Stars Ksh 500,000 kupata saini yake na kilabu chochote kinachomtaka kinafaa kuongea nayo ili imwachilie kwa njia ya maafikiano.

Katika barua yake, Sserunkuma alishukuru Gor Mahia kabla ya kuelezea dhamira yake kushiriki ligi ya Armenia inayo ng'oa nanga Januari huku kandarasi yake na mabingwa hao ikisalia miezi minane kukamilika.