SOKA-ULAYA

Karl-Heinz Rummenigge asema kumpata Messi ni kina cha maji marefu

Mwenyekiti wa Klabu ya Beyern Munich Karl-Heinz Rummenigge
Mwenyekiti wa Klabu ya Beyern Munich Karl-Heinz Rummenigge topnews.in

Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amaetolea nje jitihada za kumpata nyota wa soka anaye kipiga katika klabu ya Barcelona Lionel Messi ambaye analipwa kiasi cha Euro milioni 250 katika klabu yake.

Matangazo ya kibiashara

Rummenigge amesema kuwa kiasi hicho ni kikubwa sana kuliko hata kiasi walichotumia kumnunua Javi Martinez, na hivyo ameweka wazi kuwa hawawezi kumnunua Messi.

Aidha ameongeza kuwa anamfahamu rais wa Barcelona Sandro Rosell ambaye amekuwa rafiki yake kwa siku nyingi na kwa jinsi anavyomfahamu anaamini hawezi kumuuza Messi kwa kuwa ni mtu anayeheshimiwa katika klabu ya Barcelona.

Kumekuwa na tetesi kuhusu klabu ya Bayern Munich kutaka kumnunua Lionel Messi raia wa Argentina ambapo ikiwa jitihada hizo zitafanikiwa huenda tukashuhudia mchezaji huyo akijiunga na kocha wake wa zamani Pep Guardiola.