Michezo

Kocha wa klabu ya soka ya CS Sfaxien ya Tunisia ajiuzulu kufuatia kutolipwa marupurupu

Kocha wa klabu ya soka ya CS Sfaxien ya Tunisia ambao ni mabingwa wa taji la shirikisho barani Afrika Ruud Krol
Kocha wa klabu ya soka ya CS Sfaxien ya Tunisia ambao ni mabingwa wa taji la shirikisho barani Afrika Ruud Krol RFI

Kocha wa klabu ya soka ya CS Sfaxien ya Tunisia ambao ni mabingwa wa taji la shirikisho barani Afrika Ruud Krol amejiuzulu kwa sababu ya kutolipwa marupurupu yake tuhuma ambazo uongozi wa klabu hiyo unakanusha.

Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 64 aliamua kuacha kazi siku moja tu baada ya kufanikiwa kuishinda TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya congo kwa jumla ya mabao 3 kwa 2 mwishoni mwa juma lililopita.

Anaondoka pia akiwa ameisaidia klabu hiyo kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini humo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka minane.

Kwingineko Yaya Toure ndiye mchezaji bora wa shirika la utangazaji la uingereza la BBC baadaya kupigiwa kura na wapenzi wa soka barani Afrika.

Toure ambaye ni kiungo wa Kati ya Cote Dvoire na klabu ya Manchester City nchini uingereza aliwashinda wachezaji wengine kama Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa kunyakua taji la mwaka huu.

Toure amesema kuwa amefurahishwa mno na ushindi huo na sasa anatumai kuwa mchezaji bora wa mwaka akiwa mwafrika wa pekee aliyeorodheshwa pamoja na Lionel Messi na wachezaji wengine mashuhuri.