FIFA

Messi, Ribery na Ronald waorodheshwa kuwania tuzo ya Ballon d'Or ya FIFA kwa mwaka 2013

www.uefa.org

Lionel Messi, Frank Ribery na Cristiano Ronaldo wametajwa katika orodha ya nyota wa tatu wa kiume wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka (Ballon d'Or) kwa mwaka 2013 inayotolewa na Shirikisho la Soka duniani FIFA.  

Matangazo ya kibiashara

Messi anayeichezea klabu ya Barcelona ametwaa ubingwa ubingwa huo kwa mara nne mfululizo, lakini matumaini ya kutwaa tena taji hilo kwa mwaka huu yanafifia kutokana na kukabiliwa na majeraha msimu huu.

Winga wa Ufaransa Frank Ribery anaichezea Bayern Munich ya Ujerumani kwa mafanikio na ameiwezesha klabu yake kutwaa mataji mbalimbali likiwemo la klabu bingwa barani Ulaya.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo alitwaa taji hilo mwaka 2008 na amekuwa na matarajio huenda akatwaa tena ubingwa huo kwa mwaka huu.

Kwa upande wa walioorodheshwa kuwania tuzo hiyo ni Nadine Angerer wa Ujerumani, Marta wa Brazil na Abby Wambach wa Marekani.

Makocha wa kiume waliosalia katika orodha iliyotangazwa hii leo ni, Kocha wa zamani wa Bayern Jupp Heynckes ambaye atachuana na Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Jurgen Klopp wa Borussia Dortmund.

Kwa upande wa makocha wa kike wanaowania tuzo ni Ralf Kellermann wa VfL Wolfsburg, Silvia Neid wa Timu ya Taifa ya Ujerumani na Pia Sundhage wa Timu ya Taifa ya Uwisi.

Vinara wa tuzo hizo wanatarajiwa kutangazwa mjini Zurich tarehe 13 mwezi January mwaka 2014.