Soka-Arsenal

Wenger asema Arsenal inahitaji juhudi za ziada katika mechi ya hii leo dhidi ya Naples

Arsene Wenger Kocha mkuu wa Arsenal
Arsene Wenger Kocha mkuu wa Arsenal RFI

Timu ya Arsenal itahitaji kuweka juhudi za mwisho katika mtanange wake na timu ya Naples ambayo nayo inahitaji jitihada za makusudi kuhakikisha inafanya vizuri dhidi ya the Gunners ili kuendelea na michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa hii leo.

Matangazo ya kibiashara

Kocha wa timu ya Arsenal Arsene Wenger anakiri ugumu wa mechi hiyo na hata kutahadharisha kuwa timu ya Naple inweza ikashangaza mashabiki wa soka katika mechi ya hii leo.

Kwa upande wake, Kocha wa Naples Rafael Benitez, ametumia jana mfano wa mkulima na mwanae pamoja na punda kuelezea kuwa yeye atafanya uchaguzi wa wachezaji bila ya wasiwasi hasa kuhusu maoni ya waandishi ambao kwa siku za hivi karibuni wamelizungumzia hilo kwa hisia tofauti.