SOKA

Arsenal yatinga hatua ya mtoano ligi ya mabingwa, licha ya kichapo toka kwa Napoli

Licha ya kichapo cha magoli 2-0 toka kwa Napoli katika mechi ya jana jumatano, klabu ya soka ya Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya mtoano katika ligi ya mabingwa barani Ulaya. Mabao ya Gonzalo Higuain na Jose Callejoin yote yaliyopatikana katika kipindi cha pili cha mtanange huo hayakutosha kuiokoa Napoli ambao sasa wameyaaga mashindano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kufuzu hatua ya mtoano, Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kufadhaishwa na kikosi chake kukosa nafasi ya kuongoza kundi F ambalo kwa sasa linaongozwa na Borrusia Dortmund.

Ushindi wa Borrusia Dortmund wa magoli 2-1 katika mechi iliyopigwa dimba la Marseille umewanyima Napoli nafasi ya kutinga hatua ya mtoano.

Napoli ambayo ilichapwa mabao 2-0 na Arsenal katika mechi ya mwezi Oktoba huko London ilihitaji ushindi wa mabao matatu bila ili ijihakikishie nafasi ya kuendelea kusalia katika michuano hiyo.

Miongoni mwa vilabu vilivyofuzu katika hatua ya kumi na sita bora ni pamoja na Manchester United, Chelsea, Arsenal na Manchester City za Uingereza.

Paris Saint- Germain ya Ufaransa, Bayern munich, Schalke 04 , Bayer Leverkusen na Borrusia Dortmund za Ujerumani, Atletico Madrid, Barcelona na Real Madrid.

Michuano ya mwondoano itaanza tarehe 18 mwezi Februari mwakani na kumalizika tarehe 24.

Michuano ya robo fainali itachezwa mwishoni mwa mwezi wa tatu, huku droo ya michuano ya nusu fainali ikichezwa mwezi Aprili na fainali kuchezwa tarehe 24 katika uwananja wa Estadio da Luz jijini Lisbon nchini Ureno.