SOKA-UINGEREZA

Manchester City yapanda kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza baada ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace

REUTERS/Darren Staples

Klabu ya soka ya Manchester City imefanikiwa kupanda kileleni mwa ligi kuu ya nchini Uingereza baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace siku ya jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Bao la ushindi lilipachikwa kimiani na Edin Dzeko katika dakika ya 66 ya mchezo huo ambao ulidumisha rekodi ya City kupata ushindi katika mechi zao za nyumbani kwa zaidi ya miaka mitatu.

Wakati huo huo mahasimu wao, Manchester United nao walipata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya Norwich City.

Bao la pekee la Danny Welbeck katika dakika ya 57 limeipa Manchester U ushindi huo uliofikisha pointi 34 nyuma ya Everton ambayo nayo ina pointi 34.

Arsenal waliokuwa kileleni mwa ligi wameshuka hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi 39 nyuma ya Man City yenye pointi 41 hivi sasa.

Hii leo Arsenal itashuka dimbani kumenyana na Newcastle, Everton itakutana na Southampton, Chelsea na Liverpool wakati Tottenham Hotspurs watakuwa na kibarua dhidi ya Stoke City.