LIGI KUU UINGEREZA

Arsenal yakabiliwa na upungufu wa wachezaji nyota

Mchezaji wa kati wa Arsenal, Aaron Ramsey, atakosekana uwanjani kwa muda wa wiki tatu kwa sababu ya jeraha la mguu. Hayo ni wakati Giroud, Özil na Gibbs watakosekana kwenye mchuanao wa kesho jumatano utakaochezwa mjini Cardiff katika muendelezo wa michuano ya ligi kuu ya Uingereza, amesema leo jumanne Arsène Wenger, kocha wa Arsenal.

Matangazo ya kibiashara

"Ramsey na Ozil hawatacheza mchuano wa kesho jumatano. Ramsey ana jeraha kwa muda wa wiki tatu, na Ozil aliona daktari jana usiku lakini sina matokeo yoyote. Tulimkosa pia Gibbs na Giroud katika mechi tuliocheza naNewcastle, kwa hio tuko hapa kwa kutafakari hali hio ili tujadiliane kikosi kitakachocheza hapo kesho”, amesema Wenger.

Arsene Wenger amefahamisha kwamba Ozil , ana maumivu kwenye bega.
Giroud , mshambuliaji wa Ufaransa, atakosekana kutokana na maumivu kwenye kiwiko cha mguu aliyoyapata katika kipindi cha kwanza mechi Arsenal iliyocheza na Newcastle.

Arsene amebaini kwamba Giroud, ameanza kupata nafuu, na huenda akacheza katika mchuano kati ya Arsenal na Tottehnam utakaochezwa jumamosi ijayo.

Gibbs, winga wa kushoto, anasumbuliwa na jeraha la mguu .

Arsenal itawakosa pia Monreal na Vermaelen wa kikosi cha akiba, ambao wote ni wagonjwa. Kuna hatari Rosicky, Wilshere na Walcot wasichezi mechi hizo kutokana na majeraha waliyonayo.