LIGI KUU UINGEREZA

Arsenal yaendelea kushikilia nafasi ya kwanza baada ya kupata ushindi ambao haikua inategemea

Katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza ambayo inaendelea, Arsenal inaendelea kushikilia nafasi ya kwanza baada ya kupata ushindi wa mabao mawili kwa nunge dhidi ya Cardiff. Manchester City, ambayo inacukua nafasi ya pili kwa kushindana na Arsenal alama moja tu, iliibuka mshindi juzi jumatatu kwa kufunga mabao (3-2).

Matangazo ya kibiashara

Arsenal, ambayo imewakosa katika mchezo wake na Cardiff,wachezaji wake nyota, kama vile Özil, Ramsey na Giroud, imefaanikiwa kushikilia nafasi hii ya kwanza, baada ya Bendtner, kufaanikisha bao katika dakika ya 88.

Mchuano umekua mgumu, baada ya timu zote kuonekana kwamba zimekua zimejiadalia mechi hii.

Arsenal imekuja kuamini kua imekamilisha ushindi wake, baada ya Walcott kuchezesha wavu wa Cardiff katika dakika ya pili ya muda wa ziada.
Kwa sasa Manchester City inakuja juu kwa alama 44, na ndio tishio pekee ya The Gunners, ambayo ina alama 45.

Chelsea, 3e avec 43 points après une victoire (3-0) à Southampton qui récompense le coaching de Mourinho, complète le podium.

Chelsea inakuja na nafasi ya tatu kwa alama 43, baada ya kuiishinda Southampton mabao (3-0).

Chelsea imepata ushindi huu, baada ya kuingia uwanjani kwa Willian na Oscar, aliefunga bao la pili na la tatu, huku bao la kwanza likiwa limeingizwa wavuni na Torres baada ya kupewa pasi na kijana kutoka Brazil.