LIGI KUU UINGEREZA

Klabu ya Cardiff City baada ya kumfuta kazi Malky Mackay hatimaye imempata meneja mpya

Ole Gunnar Solskjaer, ameteuliwa kua meneja wa Cardiff City, amemurudilia Malky Mackay kwenye nafasi hii , ambae alifutwa kazi tarehe 27 desemba kutokana na kwamba mawasiliano kati yake na m'miliki wa klabu hio, Vincent Tan, hayakua mazuri, klabu ya Cardiff City imearifu katika tangazo iliyotoa jana alhamisi. 

Ole Gunnar Solskjaer, meneja mpya wa klabu ya Cardiff City
Ole Gunnar Solskjaer, meneja mpya wa klabu ya Cardiff City
Matangazo ya kibiashara

” Nimekua mwenye bahati ya kurejea kuinoa klabu ya ligi kuu. Hayo niliyaongea na familia yangu, lakini ni sifa kwangu na kujipongeza”, amesema Ole Gunnar Solskjaer, ambae aliwahi kuichezea klabu ya Manchester United, na kua mfungaji bora wa timu hio.

Solskjaer, mwenye umri wa miaka 40, alikua msimsmizi wa klabu ya Molde FK kutoka Norway katika mwaka 2010. “Hivi karibuni atafanya mkutano na waandishi wa habari”, imefahamisha klabu ya Cardiff City.

Ikiwa kwenye nafasi ya 17 ya michuano ya ligi kuu ya Uingereza, Cardiff City, mbali na masuala ya nafasi inayoshikilia, inakabiliwa na wakati mgumu kutokana na hali ya kutoelewana kati ya mashabiki na m'miliki wake.

Hali hio ya kutoelewana ilisababisha klabu hii inabadili rangi ya jezi, amabako kwa sasa klabu hii inavalia jezi za blu, wakati awali ilikua ikivalia jezi nyekundu.

Solskjaer, ambae aliichezea klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka kumi na moja, aliweza kuzingatia nasaha ya meneja wake Alex Ferguson, ambae amemtaka kukubali cheo anachopewa cha kuinoa klabu ya Cardiff City.

“ Alex Ferguson, amenitakia mafaanikio kwa kazi yangu, na amenipa nasaha ya kutosha, hasa kuzingatia kile ninachoenda kufanya”, amesema Ole Gunnar Solskjaer.